KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 20, 2011

Manuel Da Costa NDANI YA TUHUMA NZITO.


Mchezaji wa kimataifa toka nchini ureno ambae ni mzaliwa na nchini Ufaransa pamoja na klabu ya West Ham Utd Manuel Da Costa amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kumnyanyasa kijinsia msichana alie chini ya umri wa miaka 20 katika moja ya klabu ya usiku huko nchini Scotland.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amedaiwa kufanya kosa hilo Oktoba 17 mwaka jana.

Baada ya kufanya kitendo hicho Manuel Da Costa ambae tayari ameshakitumikia kikosi cha timu ya taifa ya Ureno chini ya umri wa miaka 21, aliripotiwa kwenye kituo cha polisi kilichokua karibu na klabu hiyo ya usiku, ambapo shughuli hiyo ya kushataki ilifanywa na mwandada huyo.

Hata hivyo baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo hapo jana, Manuel Da Costa ametakiwa kurejea tena mahakamani hapo Januari 25 mwaka huu, kesi yake itakapotajwa tena.


No comments:

Post a Comment