Beki wa kulia kutoka nchini Hispania Miguel Ángel "Míchel" Salgado Fernández amekubalia kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu yake ya Blackburn Rovers iliyo chini ya meneja Steve Kean kutoka nchini Scotland.
Miguel Ángel "Míchel" Salgado Fernández amekubalia kusaini mkataba wa mwaka mmoja ambao sasa utamuweka huko Ewood Park hadi mwishoni mwa msimu ujao huku dhamira yake ni kutaka kuendelea kutoa nafasi kwa vijana chipukizi kujifunza mengi kutoka kwake.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 35 tayari ameshaitumikia Rovers kwa kucheza michezo 50 toka alipojiunga na klabu hiyo mwezi August mwaka 2009 na tayari ameshapachika bao moja.
Meneja wa Rovers Steve Kean ameonyesha furaha yake kwenye mkutano wa waandishi wa habari kwa kusema kwamba ni faraja kubwa kuendelea kuwa na mchezaji huyo mkongwe ambae ana matumaini ya kuendelea kukiona kikosi chake kikifanya vyema.
Miguel Ángel "Míchel" Salgado Fernández alisajiliwa na Rovers mwaka 2009 akitokea Estadio Stantiago Bernabeu yalipo makao makuu ya klabu ya Real Madrid akiwa mchezaji huru.
.
No comments:
Post a Comment