Uongozi wa klabu ya Liverpool bado unaendeleza juhudi za kuliimarisha bechi la ufundi la klabu hiyo kufuatia hii leo kumtangaza meneja msaidizi wa zamani wa klabu ya Chelsea pamoja na West Ham Utd Steve Clarke kuwa msaidizi wa Kenny Dalglish.
Uteuzi wa Clarke, mwenye umri wa miaka 47, umechangiwa kwa kiasi kikubwa na Kenny Dalglish ambae jana alianza vibaya kibarua chake kwa kutandikwa bao moja kwa sifuri na mashetani wekundu Man Utd.
Mara baada ya kutangazwa kwa uteuzi huo Dalglish alizungumza na vyombo vya habari na kusema kwamba Steve Clarke, ni mtu muhimu sana kwake na imani yamtuma kwamba tashirikiana nae kwa ukaribu na kufikia malengo yaliyowekwa huko Anfield.
Amesema yeye binafsi pamoja na benchi zima la ufundi wanaamini kila jambo klabuni hapo litakwenda sawa huku akiwathibitishia mashabiki wa Liverpool kuendelea kuwa sambamba na Sammy Lee aliekua msaidizi wa Roy Hodgson alieondoka mwishoni mwa juma lililopita.
Katika hatua nyingine Kenny Dalglish amempinga vikali muamuzi Howard Webb kufuatia maamuzi aliyoyatoa kwenye mchezo wa jana dhidi ya kikosi chake ambacho kiliifunga safari hadi huko Old Trafford.
Amesema Webb hakukitendea haki kikosi chake baada ya kuamuru mkwaju wa panati upigwe katika sekunde 37 baada ya mtanange kuanza, huku akidai Daniel Agger hakumchezea rafu Dimitar Berbatov kama inavyodaiwa zaidi ya wachezaji hao kugongana.
No comments:
Post a Comment