KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, January 11, 2011

Goran Stevanovic KOCHA MPYA GHANA.


Goran Stevanovic kutoka nchini Serbia ametangazwa na uongozi wa chama cha soka nchini Ghana, kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa hilo ambalo ni miongoni mwa mataifa yanayosaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Afrika mwaka 2012.

Goran Stevanovic mwenye umri wa miaka 44, ametangazwa kuchukua nafasi hiyo ambayo iliachwa wazi na mserbia mwenzake Milovan Rajevac ambae aliamua kuondoka mara baada ya mkataba wake kufikia kikomo.

Taarifa zilizotolewa na uongozi wa chama cha soka nchini Ghana zimeleeza kwamba Stevanovic, ambae aliwahi kuwika na klabu ya Partizan Belgrade akicheza nafasi ya kama kiungo, atawasili nchini humo kesho kwa lengo la kukamilisha taratibu za ajira yake.

Shughuli ya kwanza kwa kocha huyo ni kuhakikisha kikosi chake kinafanya vyema kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uingereza utakaochezwa jijini London March 29 mwaka huu kabla ya kupambana na timu ya taifa ya Congo Brazzaville kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment