KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 10, 2011

Paul Jewell MBADALA WA ROY KEAN.


Uongozi wa klabu ya Ipswich Town umemtangaza Paul Jewell kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ambayo jana imepokea kisago cha mabao saba kwa sifuri toka kwa mabingwa watetezi wa kombe la FA Chelsea.

Uongozi wa klabu hiyo umemtangaza Jewell, kuwa meneja baada ya kumtimua kazi Roy Kean mwishoni mwa juma lililopita kufuatia matokeo mabovu yaliyokua yakimuandama.

Jewell amekubali kukinoa kikosi cha Ipswich Town kwa mkataba wa miaka miwili na nusu huku wengi wakimkumbuka kwa maamuzi yake ya kujiuzulu nafasi ya umeneja ndani ya klabu ya Derby County baada ya kubanjuliwa bao moja kwa sifuri na klabu yake ya sasa mwezi Disemba 2008.

No comments:

Post a Comment