KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 27, 2011

LIVERPOOL KUUWAHI MUDA WA USAJILI?


Licha ya kusalia siku nne kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili, meneja wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish bado ana matumaini ya kuuwahi muda huo kwa kufanya usajili wa wachezaji ambao watajiunga na kikosi chake.

Dalgilish ameeleza uwezekano huo, usiku wa kuamkia hii leo mara baada ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambapo amedai tegemeo lake kubwa ni kukamilisha utaratibu huo wa usajili kwa kuwapeleka wachezaji wawili wanaocheza nafasi tofauti huko Anfiled.

Amesema suala la fedha ndani ya klabu ya Liverpool sio tatizo na tayari uongozi wa juu umeshamthibitishia hilo, hivyo kilichosalia kwake ni kukamilisha utaratibu uliowekwa na kwa ajili ya kuwasajili wachezaji hao wawili.

Tayari uongozi wa klabu ya Ajax Amsterdam kupitia kwa meneja wao Frank de Boer umeshautaka uongozi wa klabu ya Liverpool kuhakikisha wanatimiza azma yao ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uruguay Luis Alberto Suárez Díaz hadi siku ya jumamosi na endapo itakua kinyume na hapo dili hilo litavunjika.

Klabu ya Liverpool pia ina mikakati ya kutaka kumng’oa Chalie Adam huko Bloomfield Road yalipo makao makuu ya klabu ya Blackpool huku ofa ya kumsajili kiungo huyo wa kimataifa toka nchini Scotland ya paund million 4 iliyowasilishwa mwishoni mwa juma lililopita ikiwa imewekwa kampuni.

Wakati huo huo Kenny Dalglish amekiri kufurahishwa na maelewano mazuri ya kiuchezaji yaliopo kati ya viungo wake Raul José Trindade Meireles pamoja na Steven George Gerrard ambao walionekana kuwa chachu ya ushindi wa bao moja kwa sifuri uliopatikana usiku wa kuakia hii leo mbele ya Fulham huko Anfield.

Amesema wachezaji hao kwa takribana majuma kadhaa yaliyopita wamekuwa wakionyesha uhalisia wa kucheza kwa kujituma pale inapotakikana na sasa mafamnikio yameanza kuonekanda ndani ya kikosi chake ambacho kinashikilia nafasi ya saba katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza baada ya mchezo wa jana.

No comments:

Post a Comment