KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 13, 2011

HISPANIA WAPO JUU ZAIDI YA UINGEREZA - BLATTER.


Raisi wa shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA Sepp Blatter ameutaka uongozi unaosimamia ligi kuu ya soka nchini Uingereza kujifunza baadhi ya mambo kutoka kwenye uongozi unaoongoza ligi kuu ya soka nchini Hispania endapo, utahitaji kutoa wachezaji bora ulimwenguini.

Blatter ametoa kauli hiyo kwa vigezo vya nchi ya Hispania kuendelea kufanya vyema katika medani ya kimataifa ambapo kwa kipindi kirefu sasa imekua ikiwatoa wachezaji bora duniani.

Amesema hakuna linaloshindikana katika suala hilo, bali kinachotakiwa ni kuigwa kwa mfumo mzuri unatumiwa na viongozi wa Hispania ambao wamekua wakijitahidi kuiboresha ligi ya LA LIGA kila mwaka na matokeo yake yanaonekana kwa kuwa na klabu bora zilizosheheni wachezaji wenye viwango vya hali ya juu.

Amesema mfumo unaotumika nchini Hispania unatoa nafasi kubwa kwa wachezaji wazawa kucheza kwa asilimia kubwa kwenye vilabu vyao mbali na ilivyo nchini Uingereza ambapo wachezaji wengi hutokea nje ya nchi hiyo.

Blatter hakusuta kumzungumzia mchezo bora wa dunia Lionel Andrés "Leo" Messi kwa kusema alistahili kutwaa tuzo hiyo siku tatu zilizopita kufuatia umahiri wake mkubwa anaouonyesha akiwa uwanjani na pengine kuisaidia klabu yake kupata ushindi kwenye michuano mbali mbali walioshiriki msimu uliopita.

Raisi huyo wa FIFA amesema Lionel Andrés "Leo" Messi hana tofauti kubwa na Dego Armando Maradona ambae nae aliwahi kuonyesha uwazo mkubwa wakati akisakata kabumbu miaka ya 80 hadi 90.

No comments:

Post a Comment