KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 13, 2011

Mario Balloteli ATACHEZA LICHA YA DZEKO KUSAJILIWA.


Meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini amewatoa wasi wasi baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo walioanza kuhoji nafasi za wachezaji wanaocheza safu ya ushambuliaji, baada ya kusajiliwa kwa Edin Zdeko akitokea Wolfburg ya nchini Ujerumani.

Mancini amewatoa wasiwasi mashabiki hao baada ya hofu kuzuka huenda mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Italia Super Mario Baletelli akakalishwa benchi na nafasi yake kupewa Edzin Dzeko alietambulishwa klabuni hapo usiku wa kuamkia jana.

Amesema yeye kama meneja anajua namna ya kuwachezesha washambuliaji hao kwa pamoja hasa ukizingatia Balotelli alipokua nchini Italia na klabu yake ya zamani ya inter Milan alikabiliwa na changamoto kubwa ya kuznguukwa na washambuliaji mahiri lakini alichezeshwa snao sambamba na timu ikafikia malengo yaliyowekwa.

Mbali na kutoa uhaikika wa kucheza pia Mancini amedai kwamba kuwepo kwa washambuliaji wazuri ndani ya kikosi chake ni ishara tosha ya kuonyesha ni vipi hawatotetereka pale mmoja atakapokua mgonjwa kama ilivyo hivi sasa kwa Balotelli ambae atakuwa nje kwa muda wa mwezi mmoja ujao.

Katika hatua nyingine Roberto Mancini amethibitisha uwezekano wa kuuzwa kwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Paraguay Roque Santa Cruz pamoja na winga wa kimataifa toka nchini Uingereza Shaun Wright-Phillips katika kipindi hiki cha mwezi januari.

Mancini amesema tayari uongozi wa klabu ya Blackburn Rovers umeshaonyesha nia ya kutaka kumrejesha Santa Cruz katika himaya ya Ewood Park, hivyo wanasubiri ofa itakayotumwa huko City Of Manchester huku klabu kama Fulham, Birmingham City pamoja na West Ham zikionyesha harakati za kutaka kumsajili Shaun Wright-Phillips.

Mancini pia akamzungumzia mshambulaiji wa kimataifa toka nchini Togo Emmanuel Sheyi Adebayor kwa kusema hana uhakika kama ataweza kumruhusu katika kipindi hiki hadi hapo hali ya Mario Balotelli itakapothibitika kuwa sawa bin sawia.

No comments:

Post a Comment