Wajumbe wawili wa shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA walioadhibiwa kwa kosa la kujihusisha na masuala la kuomba rushwa Amos Adamu pamoja na Reynald Temarii wote kwa pamoja wamekata rufaa kupinga adhabu iliyowakumba mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2010.
Amos Adamu raia wa nchini Nigeria amepinga adhabu ya kufungiwa kujishughulisha na soka kwa muda wa miaka mitatu huku Reynald Temarii raia wa nchini Tahiti akipinga kufungiwa kujishughulisha na mchezo wa soka kwa muda wa mwaka mmoja.
Kisanga kwa wajumbe hao wawili kilizuka baada ya moja ya chombo cha habari nchini Uingereza kutoa uthibitisho wa picha za televisheni ambazo zilimuonyesha Amos Adamu pamoja na Reynald Temarii wakiomba rushwa kwa wawakilishi wa nchi zilizokua kwenye mchakato wa kuwania nafasi ya kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 pamoja na 2022.
Tayari kamati ya rufaa ya FIFA inayoongozwa na raisi wa chama cha soka nchini Bermuda, Larry Mussenden imethibitisha kupokelewa kwa rufaa hizo ambazo zitaanza kusikilizwa siku zijazo kadhaa na maamuzi ya nini kimeamuliwa yatatolewa kwenye mkutano mkuu wa FIFA utakaofanyika mwezi ujo mjini Zurich nchini Uswiz.
Amos Adamu raia wa nchini Nigeria amelazimika kukataa rufa hiyo kwa lengo la kutaka kujisafisha kabla ya kuingia kwenye harakati za kutetea nafasi yake ya ujumbe kwenye mkutano wa uchaguzi wa CAF unaotarajiwa kufanyika Februari 23 mjini Khartoum nchini Sudan.
No comments:
Post a Comment