KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, January 11, 2011

Kenny Dalglish AITEGA LIVERPOOL.


Meneja wa muda wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish huenda akasaini mkataba wa kukinoa kikosi cha klabu hiyo kwa muda mrefu ujao.

Kenny Dalglish raia wa nchini Scotland, anatazamiwa kufikia makubaliano hayo baada ya kuonyesha dalili za kutaka kukubalia mkataba wa kudumu ndani ya klabu hiyo ambayo aliitumikia toka mwaka 1977-1990 akiwa kama mchezaji.

Mkurugenzi wa soka wa klabu ya Liverpool Damien Comolli amekutana na waandishi wa habari na kueleza mkakati huo ambapo amesema kwa sasa uongozi wa ngazi za juu unafikiria kufanya hivyo kwa malengo ya kuboresha mazingira ya mafanikio huko Anfield.

Alipoulizwa Dalglish juu ya mkakati huo amesema ni kweli lakini inategemea na mazuri atakayoyafanikisha hadi mwishoni mwa msimu huu.


No comments:

Post a Comment