KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 27, 2011

KUTOKA PIRATES HADI SUNDOWNS.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Afrika kusini Teko Sholofelo Modise hii leo amesushtua umma wa mashabiki wa soka nchini Afrika kusini kufuatia uhamisho wake toka kwenye klabu ya Olarndo Pirates na kujiunga na Mamelodi Sundowns.

Usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa umri wa miaka 28, umewashtua wengi nchini humo baada ya kufanywa kimya kimya baina ya viongozi wa vilabu hivyo viwili ambavyo vyote vinashiriki kwenye ligi kuu ya soka nchini Afrika kusini.

Taarifa zimeeleza kuwa Teko Sholofelo Modise ambae ni miongoni mwa wachezaji walioshindwa kuifikisha mbali Afrika kusini kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2010, tayari ameshasaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Sundowns huku kiasi cha ada yake ya uhamisho kikifanywa kuwa siri.

Taarifa hizo zimeendelea kueleza kwamba Teko Sholofelo Modise kesho atajiunga rasmi na kikosi cha Sundown mazoezini na kisha baada ya hapo atatambulishwa rasmi katika vyombo mbali mbali vya habari.

Tayari mwenyekiti wa klabu ya Orlando Pirates Irvin Khoza amethibitisha taarifa za kuondoka kwa kiungo huyo ambapo amedai Teko Sholofelo Modise siku kadhaa zilizopita aliwasilisha maombi ya kutaka kuondoka klabuni hapo nay eye bila khiyana aliridhia ombi hilo.

Hata hivyo Irvin Khoza amedai uongozi wa Mamelodi Sundowns ulitaka kukamilisha dili hiyo kwa makubaliano ya kubadilishana mchezaji sambamba na kulipa sehemu ya fedha lakini hawakuliafiki ombi hilo.

Teko Sholofelo Modise kwa upande wake amesema amefurahishwa na maamuzi ya kukubaliwa ombi lake ambalo sasa limetimiza ndoto zake.

No comments:

Post a Comment