Uongozi wa majogoo wa jiji Liverpool umetuma taarifa nchini uholanzi kwenye klabu ya Ajax Amsterdam juu ya kutaka kukamilisha taratibu zote za kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uruguay Luis Alberto Suárez Díaz.
Taarifa zilizotumwa huko Amsterdam Arena zimeutaka uongozi wa klabu hiyo ya nchini Uholanzi kuthibitisha uwezekano wa kuwa tayari kumuuza mshambuliaji huyo hadi siku ya jumamosi na kinyume na hapo dili la usajili la Suarez litavunjika.
Liverpool tayari wameshatuma ofa ya paund million 12.7 ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 lakini uongozi wa Ajax ulirejesha majibu huko Anfiled kwa kueleza kuwa kiasi hicho cha fedha hakilingani na thamani ya mchezaji huyo.
Hata hivyo tayari Luis Alberto Suárez Díaz ameshaeleza wazi nia yake ya kutaka kuelekea nchini Uingereza lakini kikwazo kikubwa kinaonekana kuwa meneja wa klabu ya Ajax Amsterdam Frank de Boer ambae anadaiwa kuwashinikiza mabosi wake kuikataa ofa iliyowasili huko Amsterdam Arena.
Luis Alberto Suárez Díaz kwa sasa bado anatumikiwa kifungo cha kutokucheza michezo kumi ya ligi kuu ya soka nchini Uholanzi, baada ya chama cha soka nchini humo kumkuta na hatia ya kumng’ata begani winga wa klabu ya PSV Eindhovein Otman Bakkal pindi timu hizo zilipokutana mwezi novemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment