Benchi la ufundi la klabu ya Chelsea linajipa matumaini ya kumtumia kiungo Frank Lampard katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza utakaochezwa mwanzoni mwa juma lijalo dhidi ya Bolton Wanderers.
Matumaini hayo ya benchi la ufundi yanakuja kufuatia kiungo huyo kukabiliwa na maumivu wa kiazi cha mguu aliyoyapata siku ya jumatano akiwa mazoezini na wachezaji wenzake.
Tayari kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, ameshafanyiwa vipimo, na majibu yameonyesha huenda ikamchukua kipindi kirefu kurejea tena uwanjani endapo atajitonesha katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mchezo huo wa mwanzoni mwa juma lijalo.
Kama itakumbukwa vyema kiungo huyo amerejea uwanjani ndani ya majuma matatu yaliyopita baada ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa ngiri ambayo humsumbua mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment