KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 20, 2011

WASHIKA BUNDUKI WA EMIRATES WALEEE !!

Leeds United 1-3 Arsenal (Agg 2-4)


Mchezo wa marejeano wa mzunguuko wa tatu wa kombe la FA kati ya Arsenal dhidi ya Leeds Utd usiku wa hii leo umechezwa kwenye uwanja wa Eland Road.

Matokeo ya mchezo huo ni kwamba washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal, wamefanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa mabao matatu kwa moja ambapo mabao hayo yamepachikwa wavuni na Samir Nasri, Bakari Sagna pamoja na Robin Van Parsie huku Jonny Howson akiwaliwaza wachezaji wenzake wa Leeds Utd kwa kupachika la kufutia machozi.

Kama itakumbukwa vyema katika mchezo wa kwanza uliochezwa huko Emirates Stadium jijini London majuma mawili yaliyopita timu hizo zilikwenda sare ya bao moja kwa moja hatua mbayo inaifanya Arsenal kusonga mbele kwa jumla ya mabao manne kwa mawili.

Kwa matokeo hayo sasa Arsenal watawakabili Huddersfield Town katika mchezo wa mzunguuko wa nne wa michuano hiyo utakaochezwa Januari 30 kwenye uwanja wa Emirates.

No comments:

Post a Comment