Shirikisho la soka nchini Sudan limetoa uthibitisho wa kukamilika kwa sehemu ya maandalizi ya michuano ya mataifa bingwa barani Afrika yalipangwa kufanyika nchini humo kuanzia Februali 4-25 mwaka huu.
Taarifa za kukamilika kwa sehemu ya maandalizi ya michuano hiyo zimetolewa na katibu mkuu wa shirikisho hilo la soka nchini Sudan Hassan Abou Bin Jabal, ambapo amesema asilimia kubwa ya maandalizi ya michuano hiyo imeshakamilika na sasa wanasubiri kukabidhiwa kila idadra mwishoni mwa mwezi huu.
Hassan Abou Bin Jabal pia amewatoa hofu mashabiki wa soka wanaotarajia kusafiri kuelekea nchini humo kuzishangilia timu zao za taifa kwa kueleza kwamba hali ya kiusalama ni shwari na hakuna shaka yoyote ambayo itajitokeza.
Nchi ya Sudan inakuwa mwenyeji wa fainali hizo za mataifa bingwa barani Afrika ambapo kwa mara ya kwanza fainali hizo zilichezwa nchini Ivory Coast mwaka 2009 kwa kuzishirikisha nchi nane ambapo miongoni mwa nchi hizo Tanzania ilikuwepo.
Katika fainali za mwaka huu, timu shiriki zimeongezeka kutoka nchi nane hadi 16 ambazo zimepangwa katika makundi manne tofauti.
No comments:
Post a Comment