KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 24, 2011

Pedro Lima ATOA PONGEZI KWA VIJANA.


Baada ya kutwaa ubingwa wa fainali za mataifa ya bara la Afrika chini ya Umri wa miaka 17, mwishoni mwa juma l;ililopita huko mjini Kigali nchini Rwanda, kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Burkina Faso Pedro Lima amesema hatua hiyo ni ishara nzuri kwa nchi yao ambayo kwa kipindi cha miaka mingi haikuwahi kufanya hivyo.

Pedro Lima amesema ushindi huo wa mabao mawili kwa moja ambao waliupata mbele ya timu ya taifa ya Rwanda iliyokua ikishanguiliwa na mashabiki wake likuki kwenye uwanja wa Amahoro haukuwa rahisi kupatikana zaidi ya wachezaji wao kufanya kazi ya ziada na kuhakikisha hatua hiyo inafanikiwa.

Amesema Burkina Faso hakuwahi kutwaa ubingwa wa soka wa aina yoyote na ubingwa huo umekua wa kwanza kwao hivyo wanauchukuliwa kama sehemu ya kupata mafanikio zaidi katika bara la afrika na nje ya bara hilo.

Burkina Faso walifanikiwa kupata ushindi huo wa mabao mawili kwa moja katika hatua ya fainali dhidi ya wenyeji Rwanda, huku wakiwa pungufu kufuatia Kanazoe Bassirou kuonyeshwa kadi nyekundu.

Mabao hayo ya Burkina Faso yaliyofungwa na Zaniou Sana pamoja Kabore Abdoul Aziz huku bao la kufutia machozi la wenyeji likifungwa na Tibingana Mwesigye.

Bingwa wa fauinali hizo za mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17 anaungana na washindi wengine wa tatu wa fainali hizo ambao ni Rwanda, Kongo Brazzaville pamoja na Ivory Coast kwenda kuwania ubingwa wa dunia nchini mexico kuanzia mwezi June-July mwaka huu.

No comments:

Post a Comment