KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 20, 2011

NGOMA NZITO KWA Essam El Hadary.


Mahakama kuu ya nchini Uswiz imemtaka kipa wa kimataifa toka nchini Misri Essam El Hadary kulilipa shirikisho la soka ulimwenguni kote dola za kimarekani 12,500 baada ya rufaa yake ya kupinga hukumu ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Sion nchini humo kugonga mwamba.

Mahakama hiyo ya ya kimichezo nachini Uswaz pia imemtaka kipa huyo mwenye umri wa miaka 38, kulipa gharama za usumbufu wa kesi yake ambapo anatakiwa kulipa franga za uswiz 10,000 pamoja na gharama za uendeshwaji wa kesi yake katika mahakama ya kimichezo ya ya FIFA ambazo ni dola za kimarekani 796,500.

El Hadary amekumbwa na mkasa huo baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Sion ambayo ilimsajili kutoka kwenye klabu yake ya zamani ya nchini kwao Misri Al Ahly mwaka 2008.

Kufuatia hatua hiyo kipa huyo alifungiwa na shiriksiho la soka duniani FIFA kwa kutakiwa kutojishughulisha na masuala ya soka kwa muda wa miezi minne ambapo adhabu hiyo yatarajiwa kumalizika mwezi ujao.

Baada ya kuamliza kifungo hicho na kulipa fedha anazotakiwa kuzilipa El Hadary ataruhusiwa kuituimikia klabu yake ya sasa ya nchini Sudan Al-Merreikh.

No comments:

Post a Comment