KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, January 14, 2011

Roque Santa Cruz AREJEA EWOOD PARK.


Klabu ya Blackburn Rovers umekamilisha dili la kumsajili kwa mara nyingine tena mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Paraguay Roque Santa Cruz akitokea Manchester City.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekamilisha usajili huo ambao unamrejesha Ewood Park baada ya kukamilisha vipimo vya afaya yake mishale ya mchana kwa saa za Afrika ya mashariki.

Mara baada ya kukamilisha taratibu za kurejea Ewood Park Roque Santa Cruz alitambulishwa kwa waandishi wa habari na kueleza kwamba anajihisi mwenye furaha ya mtu ambae amerejea tena yumbani baada ya kutoweka kwa muda mrefu.

Santa Cruz, alisajiliwa na Bluckburn Rovers mwaka 2007 akitokea Bayern Munich ya nchini Ujerumani na mwaka 2009 alijiunga na klabu ya Man city ilipokua chini ya meneja Mark hughes.

Akiwa Ewood Park kwa kipindi cha miaka miwili, mshambuliaji huyo alifanikiwa kucheza michezo 70 na kupachika mabao 29.

No comments:

Post a Comment