Wagonga nyundo wa London West Ham Utd wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kinyang’anyiro cha kuumiliki uwanja wa Olympic utakaotumika katika michuano ya Olympic ya mwaka 2012 huko jijini London.
West ham utd wanapewa nafasi hiyo kufuatia sera yao ya kutoaondoa sehemu ya kukimbilia endapo watafanikiwa kushinda kinyang’anyiro hicho, utaratibu ambao unapingana na sera ya wapinzani wao TottenHam Hotspurs ambao tayari wameshaeleza wazi nia yao ya kuondoa sehemu ya kukimbilia endapo watashinda.
Kufuatia sera hiyo, mwenyekiti wa kamati ya michezo ya Olimpiki ya jijini London mwaka 2012 Lord Coe, ameunga mkono sera ya west ham utd huku akieleza kwamba kamati yake bao ina wajibu wa kuhifadhi uwanja wa Olimpiki kuwa uwanja wa riadha na michezo tofauti.
Maamuzi ya nani atashinda katika kinyang’anyiro hicho yanatarajiwa kutolewa siku ya ijumaa kwenye mkutano wa mwisho wa kamati ya maandalizi ya michuano ya Olimpic ya mwaka 2012.
Mshindi atakaetangazwa katika maamuzi hayo atalazimika kusubiri hadi kumalizika kwa michuano wa Olympic mwaka ujao na kisho atakabidhiwa uwanja huo.
Iwapo West Ham Utd watashinda kinyang’anyiro hicho watukuwa wamehama maili mbili kutoka uwanja wao sasa Upton Park huku Spurs endapo watashinda wao watakuwa wamehama kwa urefu wa maili tano kutoka White Hart Lane.
No comments:
Post a Comment