Meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza Chelsea Carlo Ancelotti amerejea tena majivuno kwa kusema kikosi chake hakitarejea nyuma baada ya ushindi wa mabao saba kwa sifuri uliopatikana jana kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Ipswich Town.
Anceloti ametoa tambo hizo jijini London mara baada ya kikosi chake kurejea Stamford Bridge ambapo amesema ushindi wa mabao saba ni ishara nzuri ya wao kurejea kwenye mtiririko wa ushindi kama ilivyokua siku za nyuma na imani yake yamtuma hakuna kitakachowazuia kufanya hivyo.
Amesema kipimo kizuri kitaanza kuonekana mwishoni mwa juma hili kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Blackburn Rovers ambao watasafiri kuelekea Stamford Bridge.
Wakati Anceloti akirejea tambo hizo, kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza pamoja na klabu hiyo Frank Lampard nae ameelezea matarajio ya kikosi chao mara baada ya kufanya kweli katika mchezo wa jana ambao uliunguruma huko Portman Road.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 amesea walicheza vyema tena kwa kuelewana hivyo hana shaka na matarajio ya kikosi cha The Blues ambacho bado hakijapoteza muelekeao wake.
No comments:
Post a Comment