KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, January 18, 2011

Rafael Da Silva KUJADILIWA HII LEO.


Beki wa kulia wa klabu ya Man Utd Rafael Da Silva huenda akaingia kwenye matatizo ya kuaongezewa adhabu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Beki huyo wa kimataifa toka nchini Brazil anahofiwa kuiongia matatizoni kufuatia maneno makali aliyomtolewa muamuzi Mike Dean baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kabla ya kufanya maamuzi ya kutoka nje ya uwanja.

Hii leo mishale ya saa mbili usiku kwa saa za hapa nyumbani kamati ya nidhamu ya FA inakutana tena kujadili kitendo hicho na baadae kamati hiyo itatoa maamuzi rasmi juu ya beki huyo mwenye umri wa miaka 20.

No comments:

Post a Comment