KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, January 18, 2011

TWITER YAMPONZA RYAN BABEL !!


Winga wa kimataifa toka nchini Uholanzi na klabu ya Liverpool, Ryan Babel ametakiwa kulipa fainali ya paund 10,000, kufuatia kosa la kuweka picha ya muamuzi Howard Webb akiwa amevalia jezi ya klabu ya Man utd kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twiter.

Ryan Babel ametakiwa kufanya hivyo baada ya kamati ya nidhamu ya chama cha soka nchini Uingereza, kukaa na kujadilina juu ya suala hilo na mwisho wa siku ilimkuta na hatia ya kumdhalilisha muamuzi huyo kwa madai ni shabiki mkubwa wa Man Utd.

Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya Roger Burden amesema wamelazimika kumuadhibu Babel baada ya kutambua kwamba mtandao wa Twiter ni mtandao wa kijamii hivyo hakupaswa kumfanya udhalilishaji huo ambao umeonekana ulimwengu mzima.

Ryan Babel alifanya maamuzi ya kuweka picha ya muamuzi huyo kwenye mtandao wa Twiter baada ya kuchukizwa na maamuzi ya kuizawadia penati Man Utd katika sekunde ya 37 ya mchezo wa kombe la FA ambapo Liverpool walikubali kisago cha bao moja kwa sifuri lililofungwa kupitia mkwaju huo.

Hata hivyo Babel alimuomba radhi muamuzi huyo sambamba na mashabiki wa soka ulimwenguni kote kwa kitendo hicho alichokifanya.


No comments:

Post a Comment