KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 17, 2011

Samson Siasia AFANIKISHA MALENGO YAKE.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria Samson Siasia amefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika harakati zake za kuwahamasisha wachezaji wengi wa nchi hiyo kurejea nyumbani kulitumnikia taifa lao baada ya kuwa nje ya bara la Afrika kwa kipindi kirefu kilichopita.

Samson Siasia amefanikiwa katika suala hilo baada ya kufanya ziara huko barani Ulaya kwenda kuzungumza na wachezaji hao ambao wamekubalia kwa moyo thabit kurejea nyumbani na kulitumikia taifa lao katika michezo ya kimataifa.

Mmoja wa wachezaji hao waliokubali kurejea nyumbani barani Afrika ni mshambuliaji wa klabu ya Newcastle United ya nchini Uingereza Foluwashola "Shola" Ameobi ambae atajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kitakachocheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Guatemala utakaochezwa nchini Marekani mwezi ujao.

Ameobi mwenye umri wa miaka 29, aliezaliwa kusini mwa nchini Nigeria katika jimbo la Zaria, amekubali ombi la Siasia baada ya kukaa nchini Uingereza kwa kipindi miaka 16 iliyopita kufuatia kuchukuliwa akiwa kijana mdogo na kwenda kucheza soka kwenye klabu Newcastle Utd na tayari ameshaitumikia timu ya taifa ya Uingereza chini ya umri wa miaka 21.

Mchezaji mwingine aliekubali kurejea nyumbani ni winga wa klabu ya Wigan Athletic Victor Moses ambae ameshavitumikia vikosi vya timu ya taifa ya Uingereza chini ya umri wa miaka 16,17,19 na 21 na kwa sasa mshambuliaji huyo ana umri wa miaka 20.

Nae mshambuliaji wa klabu ya KARABUK - SPOR ya nchini uturuki Emmanuel Chinenye Emenike ni miongoni mwa wachezaji waliozungumza na Siasia na kufikia hatua ya kukubalia kurejea nchini Nigeria kucheza mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki mnamo February 9 huko mjini Miami.

No comments:

Post a Comment