KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 17, 2011

Kenny Dalglish AWEKA WAZI MKAKATI WAKE.


Siku moja baada ya kupata matokeo ya sare toka alipokabidhiwa jukumu hilo majuma mawili yaliyopita, meneja wa klabu ya Liverpool, Kenny Dalglish amesema hana budi kuijenga upya safu yake ya ulinzi kwa kuwatumia wachezaji waliopo kikosini kwa sasa.

Kenny Dalglish ametoa msimamo huo hii leo ambapo ameleeza kwamba anaamini wachezaji waliopo kwa sasa kikosni wana kila sababu ya kukamilisha zoezi hilo na likafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Amesema beki kama Paul Konchesky ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya kushoto hivyo anajitahidi kumrejesha katika kiwango chake cha kawaida ili aweze kusaidiana na Fábio Aurélio Rodrigues.

Amesema beki huyo toka alipokichukua kikosi cha klabu ya Liverpool amekua akionyesha kiwango duni, hatua mbayo inamafanya kumuweka benchi hadi hapo atakaporidhishwa na kiwango chake.

Mbali na beki huyo pia amedai wachezaji wengine wanaocheza nafasi ya ulinzi kama Glen Johnson pamoja na wengine wanahitaji mazoezi ya kisawa sawa kwa ajili ya kukabiliana na washambuliaji wa timu pinzani.

Katika hatua nyingine Kenny Dalglish amesema bado hajaanza majadilino na mabosi wake juu ya kufanya usajili wa wachezaji, kupitia kipindi hiki cha dirisha dogo ambacho kitafikia kikomo mwishoni mwa mwezi huu.

Amesema mengi yanazungumzwa juu ya kutaka kusajiliwa kwa wachezaji klabuni hapo lakini ukweli ni kwamba majadilino ya usajili huyo hayajaanza licha ya wachezaji kama Stephen Warnock wa klabu ya Aston Villa pamoja na mshambuliaji wa klabu ya Ajax Amsterdam Luis Suarez kuhusishwa na safari ya kutaka kuelekea Anfield.

No comments:

Post a Comment