KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 17, 2011

Steve Bruce AMUOMBA RADHI HARPER.


Meneja wa klabu ya Sunderland Steve Bruce amemtaka radhi kipa wa klabu ya Newcastle Utd Steve Harper kufuatia kitendo alichofanyiwa na shabiki anaedaiwa kuwa wa paka hao weusi mara baada ya mtanange wa jana uliopigwa huko Stadium of Light.

Bruce amelazimika kufanya hivyo baada ya kukiri kuchukizwa na kitendo hicho kilichojitokeza bila ya kutegemewa lakini akaendelea kueleza kwamba Hapaer hana budi kuwasamehe watu wa Sunderland.

Amesema mbali na kuomba radhi pia wanashukuru shabiki huyo alieingia uwanjani, hakumdhuru mchezaji huyo ambae aliekua benchi kwa kipindi kirefu kilichopita kufuatia jeraha la bega.

Hata hivyo mbali na kuomba radhi na kukilaani kitendo hicho, Steve Bruce amewapa tano mashabiki wa klabu hiyo kwa msaada wao wa kukishangilia kikosi chake ambacho kilifanikiwa kusawazisha bao katika dakika za lala salama kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ghana Asamoah Gyan.

Wakati huo huo mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ghana na klabu ya Sundeland Asamoah Gyan amekiri bao alilofunga katika mchezo huo wa jana lilikuwa kama bahati ya mtende kufuatia mpira uliopanguliwa na kipa wa Newcastle Utd Steve Harper kumgonga kifuani na kudidimia wavuni.

No comments:

Post a Comment