KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, January 18, 2011

Steven Jerome Pienaar AWEKWA NJIA PANDA.



Uhamisho wa kiungo wa kimataifa toka nchini Afrika kusini na klabu ya Everton ya nchini Uingereza Steven Jerome Pienaar umefanyiwa mapinduzi na uongozi wa klabu ya Tottenham Hotspurs baada ya hapo jana bahati hiyo kutangazwa kuangukiwa kwa Chelsea.

Tottenham Hotspurs wamefanya mapinduzi hayo, baada ya kukubali kulipa ada ya uhamisho wa mchezaji huyo kama walivyotakiwa mwanzoni na uongozi wa klabu ya Everton kwa ajili ya kumnasa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28.

Jana meneja wa klabu ya Everton David Moyes alithibitisha kuikubali ofa ya klabu ya Chelsea ya paund million 3, lakini hii leo mambo yamegeuka na sasa Steven Pienaar, atatakiwa kufanya uchaguzi wa wapi pa kuelekea kati mahasimu hao wawili wa jijini London.

Steven Pienaar aliifunga safari ya kuelekea nchini Uingereza mwaka 2008, baada ya kusajiliwa na klabu ya Everton akitokea nchini Ujerumani alipokua akiitumikia klabu ya Borussia Dortmund ambayo ilikubali kumuuza kwa ada ya uhamisho wa paund million 2.

No comments:

Post a Comment