KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, February 15, 2011

ANCELOTTI AENDELEA KUJITETEA.


Meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Michelangelo Ancelotti ameendeleza utaratibu wa kutoa maelezo ya kushindwa kuwatumia kwa pamoja washambuliaji wake wawili Fernando Torres pamoja na Didier Drogba katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo.

Carlo Ancelotti amelazimika kutoa maelezo hayo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kwa nini alishindwa kuwatumia washambuliaji hao ambao wanaaminiwa huenda wangefanya vyema endapo wangejumuishwa kikosini kwa pamoja.

Meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italia ameeleza kwamba ilimlazimu kumuanzisha Fernando Torres kwa ajili ya kutaka kutoa nafasi kwa washambuliaji wengine kupumzika na kufukiria kuwachezesha wengine katika michezo ijayo.

Hata hivyo licha ya kumuanzisha mshambuliaji huyo wa kimataifa toka nchini Hispania Carlo Ancelotti ilimlazimu kumtoa na kumpa nafasi mshambuliaji wake mwingine Didier Drogba lakini bado matokeo ya mchezo huo yalibaki kuwa sare.

Alipoulizwa juu ya maendeleo ya Fernando Torres aliemsajili kwa kiasi cha paund million 50, Ancelotti amesema mshambuliaji huyo anaendelea vyema na jana alionyesha utofauti mkubwa zaidi ya alivyocheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya klabu yake ya zamani ya Liverpool.

Katika hatua nyingine Carlo Michelangelo Ancelotti ameendelea kuonyesha kutokujiamini na suala la kutwaa ubingwa kwa mara nyingine tena msimu huu kutokana na mwenendo wa kikosi chake ambacho kwa sasa kipo nyuma kwa idadi ya point 12 dhidi ya vinara wa ligi hiyo Man Utd.

Amesema bado wanaendelea kupigana, na hatua hiyo inampa nafasi ya kufikiria wanaweza kufuatia kuridhishwa na uwezo ulioonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo dhidi ya Fulham usiku wa kuamkia hii leo.

No comments:

Post a Comment