KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, February 15, 2011

HODGSON AOMBA USHIRIKIANO WA KUTOSHA.


Meneja mpya wa klabu ya West Bromwich Albion Roy Hodgson amesema ana imani kubwa uongozi, wachezaji pamoja na mashabiki wa klabu hiyo watampa ushirikiano mkubwa katika shughuli zake klabuni hapo.

Roy Hodgson aliechukua nafasi ya Roberto Di Mateo alietimuliwa klabuni hapo mwishoni mwa majuma mawili yaliyopita ameweka wazi matarajio hayo huku akitarajiwa kuanza shughuli ya kuketi katika benchi la ufundi la West Brom mwishoni mwa juma hili.

Amesema endapo ataonyeshwa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wahusika wa klabu hiyo kuna kila sababu za kufikia malengo yaliyowekwa klabuni hapo likiwepo lengo la kuendelea kuwepo kwenye kinyang’anyiro cha ligi kuu msimu ujao.

Amesema katika sehemu yoyote yenye mafanikio inatakiwa kutambulika kwamba nyuma yake kuna ushirikiano ambao hutolewa na kila mmoja hivyo kuondoka kwa Roberto Di Mateo hakumaanishi yeye ni bora kuliko meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italia bali kinachotakiwa ni kufunguliwa kwa ukurasa mpya.

Hata hivyo meneja huyo huyo aliefungashiwa virago huko Anfield yalipo makao makuu ya klabu ya Liverpool mwishoni mwa mwezi uliopita, ameelezea kusikitishwa na hatua ya kutimuliwa kwa mameneja katika vilabu vya soka huku akigusia suala la Roberto Di Mateo ambae safari ilimkuta baada ya kupata matokeo mabovu ya kutandikwa mabao matatu kwa sifuri na klabu ya Man City.

Kibarua cha kwanza cha Roy Hodgson kitakua mwishoni mwa juma hili pale kikosi chake kitakapokua nyumbani The Harthons kikicheza na Wolverhampton Wanderers.

No comments:

Post a Comment