KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, February 25, 2011

Cheik Ismael Tioté ASAINI MKATABA MPYA.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Ivory Coast na klabu ya Newcastle Cheik Ismael Tioté amesaini mkataba mpya na klabu ya Newcastle Utd ambao utamuwezesha kusalia huko St James Park hadi msimu wa mwaka 2016/17.

Cheik Ismael Tioté amekubalia kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia klabuni hapo kufuatia mkataba wake wa sasa aliousaini mwaka jana kutarajia kufikia kikomo mwezi August mwaka huu.

Meneja wa klabu ya Newcastel Utd Alan Pardew amesema kiungo huyo aliefunga bao la kuikoa klabu yake kwenye mchezo dhidi ya Arsenal uliomalizika kwa sare ya mabao manne kwa manne amelazimika kumshawishi kuendelea kubaki St James Park kufuatia kuwepo kwenye mipango yake ya sasa pamoja ile ya baadae.

Amesema kiungo huyo aliesajiliwa klabuni hapo kwa ada ya uhamisho wa paund million 3.5 akitokea FC Twente ya nchini Uholanzi amekuwa na bidii siku zote akiwa uwanjani na kufikia hatua ya kutoa mchango mkubwa ambao hupelekea ushindi kwa kikosi chake.

Nae Cheik Ismael Tioté alipata nafsi ya kuzungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza shughuli ya kusaini mkataba mpya ambapo ameeleza kufurahishwa na hatua ya mchango wake kuonekana ndani ya kikosi cha Newcastle ambacho ameahidi kuendelea kukitumikia kwa moyo wote.

Amesema toka alipowasili klabuni hapo mwaka 2010, amekua akijifunza mambo mengi kutoka kwa wachezaji waliomzidi umri na wengine ambao wana rika sawa hivyo anaamini ujuzi alioupata kupitia hatua hiyo umemsaidia na hadi kufikia hii leo kuonekana ni mtu mwenye thamani kubwa.

Wakati kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 akionyesha hali ya kufurahishwa na kitendo cha kusaini mkataba mpya, kiungo mwenzake kutoka nchini Uingereza Kevin Anthony Jance Nolan ameonyesha kuguswa na hatua hiyo huku akimkubali kisawa sawa Cheik Ismael Tioté .

Amesema kiungo huyo amekua akisaidiana nae kwa ukaribu wanapokua uwanjani na hata wanapokua mazoezini hivyo anaamini kuendelea kubaki klabuni hapo ni sehemu tosha ya kuendelea kupangwa kwa mikakati ya kufikia malengo yaliyowekwa.

No comments:

Post a Comment