KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, February 25, 2011

Kwesi Nyantakyi AREJESHA MAJIBU.


Baada ya kushinda kiti cha ujumbe wa shirikisho la soka barani Afrika CAF kupitia kanda ya Afrika magharibi B, mwenyekiti wa chama cha soka nchini Ghana Kwesi Nyantakyi amekanusha tuhuma zinazomnyemelea ambazo zinadai kwamba alisaidia na serikali ya nchi yake kupata kiti hicho kwenye uchaguzi uliofanyika siku tatu zilizopita mjini Khartoum nchini Sudan.

Kwesi Nyantakyi anatuhumuwa kufanya ujanja huo, na baadhi ya wapinznai wake ambao wamedai mwenyekiti huyo wa GFA alitumia fedha nyingi alizowezeshwa na serikali ya nchini kwake kwa kuwahonga wapiga kura.

Akikanusha tuhuma hizo hii leo mjini Kumasi mara baada ya kurejea akitokea nchini Sudan, Kwesi Nyantakyi amesema anatambua maneno hayo yazungumzwa na watu ambao hawakupenda ashinde nafasi anayoihodhi kwa sasa hivyo amewataka waandishi wa habari wa kanda zote za bara la Afrika kulipuuzia suala hilo.

Amesema kiujumla hakuwezeshwa na yoyote kupata nafasi hiyo bali uwezo wake wa uongozi ndio uliombeba na kuwashawishi wapiga kura kumchagua hivyo anashangazwa maneno hayo aliyoyaita ya kipuuzi ni wapi yanapotokea.

Ushindi wa Kwesi Nyantakyi aliechaguliwa kukiongoza chama cha soka nchini Ghana toka mwaka 2005, unamfanya kuwa mtu wa tano kutoka nchini Ghana ambae atauwakilisha upande wa Afrika ya maghariki B kwenye vikao vya CAF.

Watu kutoka nchini Ghana waliowahi kuuwakilisha ukanda huo ni Kobina Hagan (1961-1962, Ohene Djan (1962-1966),), Nana Fredua Mensah (1968-1972) pamoja na Samuel Okyere (1990-1994).

No comments:

Post a Comment