KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, February 28, 2011

Sellas Tetteh Teivi AJIPANGA KWA MASHAMBULIZI.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda, Sellas Tetteh Teivi ametangaza hali ya hatari katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mchezo watatu wa kundi 8 wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika mwaka 2012 ambapo kikosi chake kitakutana na timu ya taifa ya Burundi.

Sellas Tetteh Teivi ametangaza hali hiyo ya hatari kufuatia kikosi cha kushindwa kufanya vyema katika michezo miwili ya kundi hilo ambapo katika mchezo wa kwanza Rwanda walipokea kisago cha mabao matatu kwa sifuri kilichotolewa na Tembo wa Afrika ya magharibi Ivory Coast na katika mchezo wa pili wa kundi hilo Benin wakaibuka na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Amavubi.

Amesema mchezo ujao dhidi ya timu ya taifa ya Burundi, ndio mchezo utakaotoa taswira ya kikosi chake wapi kinapoelekea katika michuano hiyo hivyo amedhamiria kushinda kwa hali na uwezo wa kikosi chake atakachokiita ambapo ameahidi kuwajumuisha wachezaji wote wa Rwanda waocheza soka la kulipwa.

Kocha huyo wa kimataifa toka nchini Ghana, amebainisha wazi kwamba endapo watashindwa kupata ushindi katika mpambano huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Amahoro mjini Kigali March 26 mwaka huu huenda harakati za Rwanda kucheza fainali hizo kubwa barani Afrika zikafifia.

Sellas Tetteh Teivi anajipanga kufanya vyema katika mchezo ujao, baada ya kushindwa kuwika kwenye fainali za mataifa bingwa barani Afrika zilizofanyika nchini Sudan ambapo Rwanda waliishia katika hatua ya makundi baada ya kupoteza michezo ya hatua hiyo.

Katika michezo ya hatua ya makundi Rwanda walipoteza dhidi ya Angola (1-2), kisha wakapoteza dhidi ya Senegal (0-2) na mwisho walikubalia kuchapwa na Tunisia (1-3).

No comments:

Post a Comment