
Uongozi wa klabu ya Blackpool umesema utafanikisha suala la kumsajili kwa mkopo kipa wa kimatauifa toka jamuhuri ya Ireland pamoja na klabu ya Man City Shay Séamus John James Given endapo chama cha soka FA kitakubalia ombi lao la kufanya hivyo katika kipindi hiki.
Uongozi wa klabu hiyo ya ligi kuu ya soka nchini Uiungereza unategemea kutuma maombi ya kumsajili Shay Given, kufuatia kuumia kwa kpa wao chaguo wa pili Paul Rachubka huku ikiwa tayari msimu wa dirisha dogo la usajili umeshamalizika.
Kutokana na hatua hiyo Blackpool imewalazimu kutuma maombi ya kufanya usajili wa dharura wa kuziba nafasi ya kipa huyo, haraka iwezekanavyo kutokana na hivi sasa kuwa na uhaba wa makipa klabuni hapo.
Meneja wa klabu ya Blackpool Ian Holloway, aliulizwa na waandishi wa habari juu ya jamvbo hilo katika mkutano uliopanyika jana huko Bloomfield Road, na amethibitisha ukweli wa suala hilo huku akionyesha matumaini makubwa ya kumpata Shy Given.
Amesema sababu kubwa ya kumfikiria kipa huyo mwenye umri wa miaka 34, ni kutokana na ugumu wa upatikanaji wa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Man City ambacho kwa sasa kinamtegemea sana Joe Hart.
No comments:
Post a Comment