
Huko Ashaburton Grove yalipo makazi ya jeshi la mzee Arsene Ernest Charles Wenger kuna taarifa njema kwa wale wanaohusika na jeshi hilo.
Taarifa hizo zinaeleza kwamba kiungo wa kimataifa toka nchini Ufaransa Samir Nasri ana matumaini ya kuwakabili mabingwa wa soka toka nchini Hispania FC Barcelona kwenye mchezo wa hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani ulaya siku ya jumatano.
Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Ernest Charles Wenger amesema kiungo huyo kwa sasa anaendelea na matibabu baada ya kuumia nyama za paja mwishoni mwa mwezi uliopita kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya klabu ya Huddersfield Town na tayari ameanza kuonyesha dalili za kurejea tena uwanjani.
Amesema hii leo anatarajia kupokea taarifa rasmi juu ya maendeleo ya hali ya Samir Nasri kutoka kwa daktari wa kikosi chake Colin Lewin
ambae hata hinyo mwishoni mwa juma lililopita alimuhakikishia kwamba kiungo huyo atakua na nafasi ya kuwakabili Barca kwa asilimia 50 dhidi ya 50.
Mchezo huo wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, Arsenal wataanzia nyumbani na kisha watafunga safari kuelekea mjini Barcelona kumalizia shughuli ya hatua hiyo kwa kucheza na wenyeji wao March 8.
No comments:
Post a Comment