
Meneja wa klabu ya Manchester United Sir Alexander Chapman "Alex" Ferguson ametangaza kuziondoa klabu za Chelsea pamoja na Man City kwenye mbio za kutwaa ubingwa msimu huu.
Sir Alexander Chapman "Alex" Ferguson ametangaza dhana hiyo zikiwa zimesalia siku nne kabla ya kikosi chake kuzulu jijini London kucheza na Chelsea ambao kwa sasa wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.
Amesema kwa upande wake anaona klabu zilizo kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa msimu huu ni Arsenal pamoja na Man utd ambao kwa sasa wanakimbizana kwenye kilele cha ligi ya nchini Uingereza.
Mpaka sasa Man utd bado wapo kileleni kwa kufikisha point 57 wakifuatiwa na Arsenal wenye point 56 ambapo hata hivyo washika bunduki hao wa London wapo mbele kwa mchezo mmoja.
No comments:
Post a Comment