
Mashabiki wa klabu ya Liverpool wametakiwa kuvuta subra ya kumshuhudia mshambuliaji wao mpya akianza kuitumikia klabu hiyo Andy Carroll aliesajiliwa klabuni hapo majuma mawili yaliyopita akitokea Newcastle Utd.
Ombi hilo kwa mashabiki wa klabu ya Liverpool limetolewa na meneja wao King Kenny Dalglish alipokua akijibu maswali ya waandihsi wa habari ambao walitaka kufahamu ni lini mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ataanza kuonekana akiwa amevalia jezi nyekundu.
Amesema Carroll bado anasumbuliwa na mamivu ya paja, na amekua akiendelea na matibabua mbayo kwa hivi sasa yameanza kumsaidia na kuonekana wakati wowote atarejea katika hali yake ya kawaida.
King Kenny Dalgilish pia akawazungumzia wapinzani wake ambao wanakwenda kukutana nao kesho huko Anfield Wigan Athletic, kwa kueleza kwamba wapo katika wakati mzuri na wanatambua wanakwenda kuwatembelea huku wakiwa wanachagizwa na ushindi wa mabao manne kwa matatu walioupata mbele ya Blackburn Rovers mwishoni mwa juma lililopita.
No comments:
Post a Comment