
Huko City Of Manchester meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini ametamba kikosi chake ni bora zaidi baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Aris Salonika kutoka nchini Ugiriki.
Mancini amesema kikosi chake ni bora kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa zaidi ya ilivyotarajiwa hasa ikizingatiwa kuwa msimu huu amekua na wachezaji wengi wapya ambao wanaweza kucheza kwa ushirikiano mkubwa hivyo hana budi kusema ana kikosi kinachostahili sifa ya ubora.
Amesema pamoja licha ya kutoa sifa hiyo ya ubora bado kuna wakati mwingine wamekua hawaonyeshi kiwango kizuri wanapokua uwanjani na suala hilo huwa analichukulia kama changamoto kwa kikosi kizima.
Mabao matatu yaliyofungwa na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Bosnia Edwin Dzeko pamoja na kiungo wa kimataifa toka nchini Ivory Coast Yaya Touré katika dakika ya 7, 12 na 75 yanaipa nafasi Man city kukutana na Dynamo Kiev toka nchini Ukraine kwenye hati aya 16 bora.
Mancini amekiri klabu hiyo watakayokutana nayo ni nzuri na itawapa changamoto ya kucheza kwa kujiami zaidi lakini bado akakiri kwamba yeye binafsi anajiamini kwa kuona wana uwezo wa kuivurumisha nje klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment