KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, February 11, 2011

Roy Hodgson MENEJA MPYA WEST BROM.


Hatimae uongozi wa klabu ya West Brom Albion umemtangaza mbadala wa aliekua meneja wa klabu hiyo Roberto Di Matteo ambae alitupiwa virago vyake huko The Hawthorns mwishoni mwa juma lililopita baada ya kikosi chake kukubalia kisago cha mabao matatu kutoka kwa Man City.

Mrithi wa mtaliano huyo alietangazwa mishale ya mchana wa hii leo na uongozi wa klabu hiyo ni aliekua meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 63 ametangazwa kushika madaraka hayo baada ya kukubali kusaini mkataba ambao utampa nafasi ya kudumu klabuni hapo hadi mwezi June mwaka 2012.

Sifa kubwa iliyombeba Roy Hodgson kuchukua madaraka ya kukinoa kikosi cha West Bromwich Albion ni kuwa meneja bora wa msimu uliopita baada ya kutangazwa na chama cha mameneja wa soka nchini Uingereza ambao waliridhishwa na umahiri wake wa kukiongoza vyema kikosi cha Fulham hadi kwenye hatua ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kabla ya kufungwa na Atletico Madrid ya nchini Hispania.

Hata hivyo mapema hii leo kocha wa kikosi cha kwanza cha klabu ya West Bromwich Albion ambae alipewa jukumu la kuwa meneja wa muda Michael Appleton alieleza wazi dhamira yake ya kuwa tayari kupewa jukumu hilo moja kwa moja kufuatia kujiona ana sifa zote za kumuwezesha kutwaa nafasi hiyo.

Michael Appleton alieleza wazi namna alivyoweza kukiandaa kikosi chake kabla ya mpambano wa kesho dhidi ya West Ham Utd, ambapo amesema kila jambo lipo sawa na shughuli yake itaanza kuonekana hiyo kesho ambapo atakuwa kiongozi wa benchi la ufundi.

No comments:

Post a Comment