
Kampuni ya Olympic Park Legacy (OPLC), imeitangaza klabu ya West Ham United kuwa mshindi wa ombi la kuumiliki uwanja wa Olympic mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Olympic ya mwaka 2012 iliyopangwa kufanyika jijini London.
Kampuni hiyo imeitangaza klabu ya West Ham Utd kuumiliki uwanja huo uliopo eneo la mashariki mwa jiji la London, baada ya kuridhishwa na maelezo ya maombi ya klabu hiyo yaliyowasilishwa miezi kadhaa iliyipoita.
Sifa kubwa iliyowapa West Ham Utd nafasi ya kushinda kinyang’anyiro hicho ni maelezo ya kutokuondoa sehemu ya kumkimbilia ya uwanja huo ambao bado utaendelea kutumika kwa ajili ya michezo mingine baada ya mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2012 kumalizika.
Meneja wa klabu ya West Ham Utd Avram Grant kabla ya kutangazwa kwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho alizungumza na waandishi wa habari na kuonekana kuipigia upatu sana klabu hiyo ambapo alieleza wazi kwamba hatua hiyo itatoa nafasi ya kusonga mbele kwa The Hammers ambao hawahitajui kujenga uwanja mwingine huko magharibi mwa jiji la London.
Uwanja wa Olympic wa jijini London pia ulikua unawaniwa na klabu ya Tottenham Hotspurs ambayo ilijisumu yenyewe kufuatia maelezo yake ya kuwa tayari kuondoa sehemu ya kukimbilia endapo wangepata nafasi ya kuumiliki.
Hata hivyo haki za uwanja wa Olympic bado zitaendelea kuwa mikononi mwa serikali ya nchini Uingereza mbayo sasa itaingia makubaliano maalum na uongozi wa klabu ya West Ham Utd juu ya uendeshwaji wa uwanja huo .
No comments:
Post a Comment