KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, March 12, 2011

BABU ALAANI RAFU ALIYOCHEZEWA NANI.


Meneja wa klabu ya Man Utd Sir Alexander Chapman "Alex" Ferguson amekilaani kitendo cha beki wa klabu wa Liverpool James Lee Duncan "Jamie" Carragher cha kumchezea ndivyo sivyo winga wake wa kimataifa toka nchini Ureno Luís Carlos Almeida da Cunha Nani pindi timu hizo zilipokutana mwishoni mwa juma lililopita.

Sir Alexander Chapman "Alex" Ferguson amesema kitendo hicho alichofanyiwa mchezaji wake cha kuchezewa rafu mbaya katu hakiwezi kufumbiwa macho na yoyote yule anaefuatilia mchezo wa soka duniani hivyo hadhani kama amekosea kukilaani.

Amesema kimazingira ya kawaida beki wa klabu ya Liverpool James Lee Duncan "Jamie" Carragher alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu na muamuzi aliechezesha mchezo huo lakini cha kushangazwa aliachwa na kuonyeshwa kadi ya njano.

Hata hivyo mzee huyo wa miaka 69 ameongeza kwamba pamoja na kusema hayo yote bado suala hilo litabaki kama lilivyo sasa na hana budi kufungua ukurasa mpya huku akimtakia kila la kheri Luís Carlos Almeida da Cunha Nani ili aweze kurejea tena uwanjani kama anavyotarajiwa.

Luís Carlos Almeida da Cunha Nani tayari ameshafanyiwa vipimo na imebainika kwamba itamchukua muda wa mwezi mmoja kurejea tena uwanjani.

No comments:

Post a Comment