
Wawakilishi wa bara la Afrika katika fainali za kombe la dunia za wanawake zitakazochezwa mwezi june mwaka huu huko nchini Ujerumani mwezi June timu ya taifa ya Nigeria, wanatarajia kuanza kucheza michezo ya kimataifa ya kirafiki kuanzia mwishoni mwa juma lijalo.
Kocha mkuu wa timu hiyo iliyoingia kambini mwishoni mwa juma lililopita Eucheria Uche amesema wanaendelea vyema na maandalizi yao na wana imani kila kitu kitakwenda sawa kabla ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ethiopia mwishoni mwa juma lijalo.
Amesema kila mchezaji aliemuita kikosini anaonekana mwenye furaha hali ambayo inampa nafasi ya kutamba kufanya vizuri katika mchezo huo wa kirafiki utakaochezwa huko nchini Ethiopia.
Amesem dhumuni kubwa ya kuingia kambini mapema ni kutaka kutoa nafasi kwa kila mchezaji aliemuita kikosini kuzoea mazingira ya kambi pamoja na kufahamu mifumo mbali mbali aliyoiandaa kupitia mpango wake ambao anaamini utawasaidia kwenye fainali za kombe la dunia.
Timu ya taifa ya Nigeria itafungua fainali za kombe la dunia kwa kucheza na timu ya taifa ya Ufaransa mnamo June 26, wakifuatia mchezo wa pili kwa kucheza na wenyeji ujerumani June 30, na kisha baada ya hapo watamaliza michezo ya hatua ya makundi kwa kucheza na timu ya taifa ya Canada July 5.
Timu ya taifa ya Nigeria ilipata nafasi ya kuliwakilisha bara la Afrika kwenye fainali hizo za kombe la dunia baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa barani humo kwenye fainali zilizofanyika nchini Afrika kusini mwishoni mwa mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment