KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 18, 2011

Karl-Heinz Rummenigge Vs Miroslav Klose.


Mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha taarifa za kuwa katika mazungumzo na mshambuliaji wa klabu hiyo Miroslav Klose ambae yu njia panda katika harakati za kuendelea kubaki huko Allianze Arena.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa toka nchini Ujerumani yu katika mazungumzo hayo kufuatia mkataba wake wa sasa kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu huku uongozi wa klabu ya Beyern Munich akitaka kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja hatua ambayo anaipinga vikali kwa kutaka apewe mkataba wa miaka miwili.

Hata hivyo bado inaelezwa kwamba uongozi wa Bayern Munich unaendelea kumsisitiza mshambuliaji huyo kusaini mkataba wa mwaka mmoja kama wanavyotaka na kama itashindikana huenda wakampa ruhusa ya kuondoka na kusaka masiha sehemu nyingine.

Miroslav Klose tayari ameshaanza kuhusihwa na safari ya kutaka kuelekea nchini Italia ama Hispania kufuatia taarifa zinazodai kwamba klabu za AC Milan pamoja na Valencia zinapigana vikumbo kuiwania saini yake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

No comments:

Post a Comment