KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 25, 2011

Andrea Pirlo AIHAMA RASMI AC MILAN.


Kiungo wa kimataifa toka nchini italia Andrea Pirlo ameihama rasmi klabu bingwa nchini humo AC Milan baada ya kuthibitika amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Juventus.

Andrea Pirlo amechukua maamuzi hayo ikiwa ni majuma mawili toka aliposhindwa kuafikiana na uongozi wa klabu ya AC Milan ambao ulikua ukisita kumpatia mkataba mpya kufuatia mkataba wake wa sasa kufikia kikomo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 imebainika amaihama AC Milan kufuatia taarifa zilizochapishwa kwenye mtandao wa Juventus ambazo zimeeleza kuwa Andrea Pirlo amesaini mkataba wa miaka mitatu na uongozi wa klabu hiyo ya mjini Turine ambao utafikia kikomo June 30, 2014.

Kusajiliwa kwa kiungo huyo huko Stadio Olimpico di Torino, kuanaashiria kiungo wa nchini Italia Alberto Aquilani aliekua akiichezea Juventus kwa mkopo kurejea katika klabu yake ya Liverpool ya nchini Uingereza.

Wakati huo huo uongozi wa klabu ya Ac Milan umekamilisha utaratibu wa kumsajili moja kwa moja kiungo wa kimataifa toka nchini Ghana Kevin-Prince Boateng ambae alikua akiichezea klabu hiyo kwa mkopo toka mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2010-11.

Makamu wa raisi wa AC Milan Adriano Galliani amesema usajili wa kiungo huyo umekamilika kufautia makubaliano maalum yaliyofikiwa kati yao pamoja na viongozi wa Genoa waliokua wakimiliki Kevin-Prince Boateng, toka mwaka 2010 baada ya kumsajilia akitokea Portmouth ya nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment