KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 19, 2011

Andrea Pirlo KUONDOKA AC MILAN.


Licha ya kuwepo kwa taarifa za baadhi ya wachezaji wa klabu bingwa nchini Italia AC Milan kufikiriwa kusaini upya mikataba yao, imethibitika kwamba kiungo Andrea Pirlo ataondoka huko San Siro mwishoni mwa msimu huu mara baada ya mkataba wake wa sasa kufikia kikomo.

Andrea Pirlo ambae jana alijumuishwa katika orodha ya wachezaji wanaosubiri kupewa mikataba mipya klabuni hapo amesema hana namna ya kusubiri utaratibu huo zaidi ya kufanya maamuzi ya kuondoka baada ya kuitumikia Ac Milan kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Amesema mchango wake mkubwa alioutoa klabuni hapo anaamini unatosha na daima ataendelea kuyakumbuka mazingira ya klabu hiyo kongwe nchini Italia pamoja na barani Ulaya kwa ujumla kufuatia kujifunza mengi akiwa kama mchezaji alipata mafanikio makubwa.

Andrea Pirlo aliingia katika hali ya sintofahamu ya kupewa mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo, baada ya kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu hatua ambayo ilimpa nafasi finyu ya kujumuishwa kwenye kikosi cha meneja Massimiliano Allegri aliepewa jukumu la kukinoa AC Milan mwanzoni mwa msimu huu.

Kama itakumbukwa vyema uongozi wa AC Milan jana ulikamilisha taratibu za kumsainisha mkataba mpya kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi Mark van Bommel pamoja na beki wa kimataifa toka nchini Brazil Thiago Silva.

No comments:

Post a Comment