KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 19, 2011

Diego Ribas da Cunha KUONDOKA Volkswagen Arena?


Meneja wa klabu ya VFL Wolfsburg Felix Magath amesema huenda kiungo wa klabu hiyo Diego Ribas da Cunha msimu huu ukawa wa mwisho kwake ndani ya klabu hiyo iliyo na maskani yake makuu huko Volkswagen Arena.

Felix Magath ametoa msimamo huo baada ya kuchukizwa na kitendo kilichoonyeshwa na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 mwishoni mwa juma lililopita cha kujitenga na wachezaji wenzake baada ya kuachwa kwenye kikosi kilichocheza mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Hoffenheim .

Kufuatia hatua hiyo moja ya chombo cha habari nchini Ujerumani kimefanya mahojiano na mwenyekiti wa klabu ya VFL Wolfsburg Dr Francisco Javier Garcia Sanz, kwa ajili ya kutaka kufahamu ukweli wa jambo hilo ambalo limewashtua wengi.

Dr Francisco Javier Garcia Sanz amesema wao kama viongozi wasingependa kutia neno lolote katiak harakati hizo zaidi ya kuheshimu maamuzi ya meneja wao Felix Magath ambae ana jukumu la kumuuza Diego Ribas da Cunha ama kumuacha aendelee kuwa miongoni mwa wachezaji wake msimu ujao.

No comments:

Post a Comment