KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 24, 2011

CARLO ANCELOTTI ATABIRIWA MAZURI NA BOSI WAKE WA ZAMANI.


Makamu wa raisi wa klabu bingwa nchini Italia AC Milan Adriano Galliani amesema licha ya aliekua meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti kutupiwa virago vyake mwishoni mwa juma lililopita bado anaamini meneja huyo ana nafasi kubwa ya kupata kibarua kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Adriano Galliani ambae alikua bosi wa zamani wa meneja huyo wa kitaliano ameeleza hatua hiyo akiwa mjini Milan alipotakiwa kuzungumzia hatua ya kutimuliwa kazi kwa Ancelotti ambapo amesema hakurahishwa na utaratibu huo lakini anaamini bado umahiri na ujuzi wa Ancelotti utaendelea kuwa pele pale.

Amesema hakuna alichokosea Carlo Ancelotti akiwa na Chelsea na pengine alistahili kupongezwa kwa juhudi zake binafsi ambazo ziliiwezesha klabu hiyo kufanya vyema na kumaliza katika nafasi ya pili.

Wakati Carlo Ancelotti akitabiriwa mazuri ndani ya siku kadhaa zijazo mshambulaiji wa kimataifa toka nchini Italia pamoja na klabu ya As Roma Francesco Totti amesema anaamini meneja huyo atajiunga nae huko Stadio Olympico kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.

Francesco Totti amesema siku kadhaa zilizopita alipata nafasi ya kuzungumza na Carlo Ancelotti kwa njia ya simu na alimuahidi atakaporejea nchini Italia kwa ajili ya likizo atamtafuta na kuzungumza nae mawili, matatu hivyo anaamini umewadia wakati wa kufanya hivyo huku akiwa hana majukumu na klabu ya chelsea.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 mwanzoni mwa mwaka huu alishawahi kutangaza hadharani kwamba atakua tayari kutangaza maamuzi ya kustahafu soka lake pale atakapopata nafasi ya kufundishwa na Ancelotti angalau kwa msimu mmoja.

Klabu ya AS Roma kwa miezi kadhaa sasa imekua chini ya meneja wa muda Vincenzo Montella ambae aliombwa kufanya hivyo baada ya kujuuzulu kwa aliekua meneja klabuni hapo Claudio Ranielli.

Wakati huo huo umoja wa mameneja wa vilabu vya ligi kuu ya soka nchini Uingereza umeonyesha kusikitishwa na hatua ya kutimuliwa kazi kwa Carlo Ancelotti huku ukikiri kukunwa na uwezo wake wa ufundishaji toka alipotua nchini humo mwaka 2009.

Masikitiko ya umoja huo yameonyeshwa wakati wa tafrija fupi ya kuwapongeza mameneja wa vilabu vilivyoshiriki ligi kuu msimu wa mwaka 2010-11 ambayo ilifanyika jana jijini London.

Kwa niaba ya uongozi pamoja na mameneja wote wa vilabu vya ligi kuu , meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza Man Utd Sir Alex Ferguson alichukua jukumu la kuwasilisha maneno mazuri ya kumkubali Carlo Ancelotti ambae nae alihudhuria sherehe hizo ambazo pia zilitumika kumtangaza meneja bora wa msimu.

Roy Hodgson meneja wa klabu ya West Bromwich Albion kwa upande wake akazungumzia masikitiko yake binafsi kufuatia maamuzi ya kumfuta kazi Ancelotti yaliyochukuliwa na mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich.

Roy Hodgson amesema Carlo Ancelotti alikua bado anastahili kuendelea kuwepo klabuni hapo hasa baada ya kupata mafanikio makubwa katika msimu wake wa kwanza kufuatia kutwaa ubingwa wa ligi pamoja na ule wa kombe la FA na pia alimfahamu kitambo toka akiwa nchini Italia.

No comments:

Post a Comment