KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 24, 2011

KIKOSI CHA ITALIA CHATAJWA.


Jina la mshambuliaji wa klabu ya Man city Super Mario Balotelli pamoja na kiungo aliemaliza muda wake wa kuitumikia klabu ya Ac Milan Andrea Pirlo ni miongoni mwa majina makubwa yaliyotajwa kwenye kikosi cha nchi hiyo ambacho kitarejea katika kampeni ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya June 3 kwa kupambana na timu ya taifa ya Estonia.

Wachezaji hao wawili wameitwa katika timu ya taifa ya Italia na kocha mkuu Cesare Prandelli baada ya kukosekana kwa kipindi kilichopita kufuatia majeraha yaliyokua yakiwakabili.


Wachezaji wengine waliojumuishwa kikosini na kutoa mshangao kwa walio wengi ni nahodha wa klabu ya Sampdoria iliyoshuka daraja msimu huu Angelo Palombo pamoja na beki wa klabu ya Fiorentina Alessandro Gamberini.

Kikosi kamili cha timu ya taifa ya Italia kilichoitwa na kocha mkuu Cesare Prandelli kwa upande wa:

Makipa: Gianluigi Buffon (Juventus), Salvatore Sirigu (Palermo), Emiliano Viviano (Bologna)

Mabeki: Davide Astori (Cagliari), Federico Balzaretti (Palermo), Mattia Cassani (Palermo), Giorgio Chiellini (Juventus), Domenico Criscito (Genoa), Alessandro Gamberini (Fiorentina), Christian Maggio (Napoli), Andrea Ranocchia (Inter Milan)

Viungo: Alberto Aquilani (Juventus), Claudio Marchisio (Juventus), Riccardo Montolivo (Fiorentina), Thiago Motta (Inter), Antonio Nocerino (Palermo), Angelo Palombo (Sampdoria), Andrea Pirlo (AC Milan)

Washambuliaji: Mario Balotelli (Manchester City), Antonio Cassano (Milan), Alberto Gilardino (Fiorentina), Sebastian Giovinco (Parma), Alessandro Matri (Juventus), Giampaolo Pazzini (Inter), Giuseppe Rossi (Villarreal)

No comments:

Post a Comment