KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 26, 2011

David de Gea AIKANA SAFARI YA OLD TRAFFOLD.


Siku moja baada ya kuthibitika yu njiani kujiunga na mabingwa wa soka nchini Uingereza Man Utd, kipa wa kimataifa toka nchini Hispania pamoja na klabu ya Atletico Madrid David de Gea amekanusha taarifa za kukamilika kwa utaratibu wa yeye kuelekea huko old Trafford.

David de Gea amekanusha taarifa hizo huku akidai kwamba bado hajakamilisha taratibu za kujiunga na klabu hiyo ya mjini Manchester hivyo mashabiki wa soka ulimwenguni kote wanastahili kutambua kwamba mpaka sasa ni mali ya Atletico Madrid yenye maskasni yake huko Estadio Vicente Calderón.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 21anapigiwa upatu wa kuelekea old Traffold katika kipindi hiki kwa ajili ya kurithi nafasi inayoachwa wazi na kipa wa sasa wa man Utd Edwin Van der Sar atakaetundika gloves mara baada ya mchezo wa hatua ya fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya utakaopigwa siku mbili zijazo huko jijini London kwenye uwanja wa Wembley.

No comments:

Post a Comment