KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 19, 2011

Raphael Varane ASAKWA KWA UDI NA UVUMBA HUKO OLD TRAFFOLD.


Beki wa kimataifa toka nchini humo pamoja na klabu ya Lens Raphael Varane anaripotiwa kuwa katika harakati za kujiunga na klabu bingwa nchini Uingereza Man Utd kwa ada ya uhamisho wa paund million 9.

Taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la kimichezo la nchini Ufaransa la kila siku liitwalo L'Equipe zimeeleza kwamba beki huyo mwenye umri wa miaka 18 amemvutia meneja wa Man utd Sir Alexander Chapman "Alex" Ferguson ambae msimu ujao atataka kuboresha safu yake ya ulinzi.

Taarifa hizo zimeongeza kuwa mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa ligi ya nchini Ufaransa kati ya Lens dhidi ya AS Monaco mchezaji huyo alikua akifuatiliwa na wawakilishi wa klabu ya Man Utd.

Hata hivyo huenda Man Utd wakapata upinzani mkali katika harakati za kuiwania saini ya beki huyo kufuatia uongozi wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa kutangaza nia ya kutaka kumsajili kinda huyo kwa ajili ya msimu ujao.

Wakati huo huo mtendaji mkuu wa klabu ya Man Utd David Gill amewataka mashabiki wa klabu ya Man utd kutegemea ujio wa wachezaji ama mchezaji mpya katika klabu yao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Amesema hatua ya kutarajia kuondoka kwa wachezaji kama Edwin van der Sar, Gary Neville, Paul Scholes, Michael Owen, Wes Brown pamoja na Owen Hargreaves, inatoa nafasi kwa uongozi wa klabu hiyo kufikiria kuwaerudisha wachezaji waliouzwa kwa mkopo sambamba na kuongeza wengine katika kipindi cha usajili.

No comments:

Post a Comment