KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 27, 2011

DIRISHA LA KUPOKEA RUFAA LIMEFUNGWA CAF.


Klabu bingwa barani Afrika TP Mazembe kutoka jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, imeshindwa kuuwahi muda wa kukata rufaa inayopinga kuondoshwa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika katika msimu wa mwaka 2010-11.

Hatua ya kuchelewa kwa kukatwa rufaa ya kupinga maamuzi hayo imetangazwa na mkurugenzi wa mawasiliano wa shirikisho la soka barani Afrika CAF Suleiman Habuba ambapo amesema hawana muda kwa sasa kuipokea rufaa ya mabingwa hao mara mbili wa barani Afrika.

CAF walifikia maamuzi ya kuiondosha TP Mazembe katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika msimu huu, kufuatia rufaa iliyokatwa na viongozi wa klabu ya Simba ya nchini Tanzania kwa kupinga uhalali wa mchezaji Janvier Besala Bokungu ambae alichezeshwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa mjini Lubumbashi.

Maelezo yaliyowasilishwa katika rufaa ya klabu ya Simba ya Tanzania huko CAF yalithibitisha wazi kwamba Janvier Besala Bokungu hakuwa mchezaji halali wa klabu hiyo ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, kufuatia kuihama klabu yake ya Espirance ya nchini Tunisia Kinyemela.

Hata hivyo raisi wa TP Mazembe Moise Katumbi amepinga madai hayo ambapo amesema hakuna ukweli wowote juu ya suala hilo na kwa hivi sasa wanajipanga kwenda katika mahakama ya kimichezo *CAS* iliopo mjini Zurich nchini Uswiz kudai haki yao.

No comments:

Post a Comment