KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 26, 2011

HIDDINK AKAIANA CHELSEA.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uturuki Guus Hiddink amesema hana mpango wowote wa kutaka kujiunga na klabu ya Chelsea licha ya kuendelea kuhusishwa na taarifa za kuhitajika ndani ya klabu hiyo ambayo mwishoni mwa juma lililopita ilimtimua kazi Carlo Michelangelo Ancelotti.

Guus Hiddink amekanusha taarifa hizo alipokua akihojiwa na kituo cha televisheni cha nchini Uholanzi ambapo amesema kwa sasa ana majukumu mazito ndani ya timu ta taifa ya Uturuki hivyo hana budi kushughulika na shughuli iliyo mbele yake.

Amesema jukumu zito alilokua nalo kwa sasa ni kuhakikisha anaipelekea timu ya taifa ya Uturuki katika fainali za mataifa ya barani ulaya za mwaka 2012 kwa kuhakikisha anashinda michezo ya hatua ya kwanza ambayo itaendelea mwishoni mwa juma lijalo.

Timu ya taifa ya Uturuki mwishoni mwa juma lijalo itashuka dimbani kupambana na timu ya taifa ya Ubelgiji.

No comments:

Post a Comment